Marehemu Kanumba
GARI la aliyekuwa staa wa filamu Bongo Steven Kanumba aina ya Toyota
Land Cruiser V 8, imeelezwa linapigwa bei na limeshindikana kuuzika kwa
sababu ya bei kuwa kubwa ukilinganisha na hali ya mkoko wenyewe ilivyo
kwa sasa.
Habari za ndani kutoka kwa chanzo chetu zinasema kwamba, mteja aliyekuwa
akitegemewa zaidi ni msanii maarufu nchini, Mahsein Awadh ‘’ ambaye
baada ya kutajiwa bei alipewa kwa ajili ya kulifanyia majaribio.
CHANZO KINATIRIRIKA
Kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini chanzo hicho kilitiririka
kuwa, si kweli kuwa Dk. Cheni alipewa lile gari ili alitumie kwa muda
kufanya vifaa visiharibike bali alikuwa akilijaribu.
“Unajua ndugu yangu lile gari wenyewe (familia ya Kanumba) wanaliuza
milioni 40, Cheni amelikagua sana akagundua lina matatizo mengi ndiyo
maana akawaambia atoe milioni 25 wamekataa na sasa limemshinda na
ameshalirudisha,” kilipasha chanzo.
MATATIZO YENYEWE
Kikiendelea kutambaa na mistari, chanzo hicho kilitaja baadhi ya
matatizo ya gari hilo, kikasema: “Kwanza namba zake za usajili ni za
zamani ni T 750 AER, gia boksi ina matatizo ambayo yamesababishwa na
gari hilo kutumika likiwa kwenye four wheel ndiyo maana gia boksi
imepata matatizo.
“Halina motor vehicle, steeling power mbovu, halina road licence na
mbaya zaidi kwa namna lilivyo kwa mizunguko ya kawaida mjini, kwa siku
linatumia mafuta ya laki moja.
Vyote hivi Dk. Cheni aliviorodhesha na kwenda kuwaeleza ili wapunguze
bei lakini wamegoma, wanataka milioni 40 wakati Cheni ameng’ang’ania
kuwa anataka kutoa 25 (milioni).”
DK. CHENI KIZIMBANI
Baada ya kupata maelezo haya kutoka kwa chanzo, Ijumaa lilimvutia waya
Dk. Cheni na kumuuliza juu ya madai hayo, alisikiliza kwa makini sana
maelezo yote hadi mwisho, alipotakiwa kujibu, akakata simu kisha akazima
kabisa
0 comments:
Post a Comment