Chuo Kikuu cha St John’s Dodoma chafungwa


Chuo Kikuu cha St John’s cha mkoani Dodoma kimefungwa baada ya wanafunzi kususia mitihani wakipinga unyanyasaji wanaofanyiwa na wahadhiri.

Wanafunzi hao wanawatuhumu waalimu wao kuwa wanawaangusha kwenye mitihani na baadhi wanabaka wanafunzi wa kike.

Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Gabriel Mwaluko, wanafunzi zaidi ya 290 wamesimamishwa masomo baada ya kukiuka sheria na kugomea mitihani na hivyo chuo kimefungwa kikisubiri taratibu za kinidhamu kuchukuliwa na uongozi.

Awali uongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo ulieleza kuwa wanafunzi 290 wa St John’s na vyuo vikuu vishiriki vya Dar es Salaam, walisimamishwa masomo na uongozi wa chuo hicho uliwapa barua za kuwaondoa chuoni kuanzia wiki hii.
Habari hizo zilisema wanafunzi 196 wanaosoma Dodoma na wengine 94 wanaosoma katika vyuo vishiriki vya St. Mark's na Town Centre vya jijini walipewa barua za kuondolewa chuoni.

Rais wa serikali ya wanafunzi, Andrew Chiduo, akizungumza na NIPASHE Jumapili, alisema hatua ya kuwasimamisha inalenga kuwatisha ili kuendelea kuwalinda walimu wanaodaiwa kuwanyanyasa na kuwadhalilisha na kwamba wanasusia kufanya mitihani inayofanyika mwezi huu.

Chiduo alisema wahadhiri wanalazimisha kufanya ngono na wanafunzi wa kike, kuwabaka na wale wanaokataa wanaangushwa kwenye mitihani.

Alisema katika tukio la hivi karibuni muhadhiri (jina tunalo) alituhumiwa kumbaka mwanafunzi baada ya kumhadaa kumpa mitihani mingine baada ya kushindwa ile aliyofanya mhula uliopita.

Alisema wamelazimika kugomea mitihani baada ya mhadhiri mmoja (jina linahifadhiwa) kuwafelisha kwa makusudi wale wanaochukua kozi ya biashara wa mwaka wa kwanza huku akiwapa vitisho.

Akijibu tuhuma hizo Profesa Mwaluko alisema madai ya mwalimu kumbaka mwanafunzi yanachunguzwa kwa kuwahusisha polisi, kadhalika alisema mhadhiri anayetuhumiwa kuwafelisha wanafunzi madai yake yanafuatiliwa pia.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment