Belle9: Nitafanya kazi kimataifa

 

 


MSANII kinda kutoka Mji kasoro  Bahari(Morogoro) Belle 9, ametangaza kujipanga kuvuka mipaka kwa kufanya kazi na wanamuziki wa kimataifa.

Belle 9, aliyejitambulisha kimuziki kupitia vibao vyake ‘Sumu ya penzi’, Masogange’ na baadaye kudhihirisha uwezo wake na kibao cha ’wewe ni wangu’ aliweka wazi mipango hiyo katika mahojiano maalumu na gazeti hili wiki hii.
“Nimeshatuma ‘application’ ya kufanya kazi na wasanii wa mbele kwa ajili ya kuvuka boda, Casidy ni mwanamziki ninayemkubali sana, ninachofikiria ni kuufanya muziki wangu kuwa wa kimataifa,”alisema Belle.
Msanii huyo ambaye jina lake halisi lililopo pia katika kitambulisho cha Mpigakura ni Abelnego Damian alisema kwamba, sasa anahitaji kufanya kazi na wanamziki wa kimataifa.
Belle, anayeimba nyimbo zenye vionjo vya kimapenzi Jumapili iliyopita alizindua nyimbo yake mpya inayojulikana kwa jina na  ‘listen’ alibainisha kuwa mipango anayoitekeleza sasa ya kufanya kazi na wasanii wa kimataifa aliianza miaka mitatu iliyopita.  “Mpaka sasa nimeshafanya mawasiliano ya kufanya kazi pia na Browman na Sablos Spire kupitia mawakala wao,”anasema Belle 9.
Anaeleza kuwa juhudi za kuwasiliana na wasanii hao  anazifanya kupitia kwa rafiki yake, Johnson Elias anayeishi nchini Australia kwa muda mrefu sasa.
“Huyu ndiye anayefanya mipango yote huko, huwa nawasiliana naye kwa kila hatua anayofikia, sina mashaka kabisa. Ninachoamini, siku moja nitafanya nao kazi studio,”anasema Belle 9 kwa matumaini.
Anasema kuwa kwa mujibu wa taarifa anazozipata kutoka kwa rafiki yake Johnson, maombi yake ya kufanya kazi na wasanii hao zinamjengea matumaini.
“Johnson ananiambia kuna mazingira magumu kidogo kwa sasa, ila taarifa zangu walizipokea freshi, ila muda mwingi wanabanwa na ratiba za shoo,”anasema Belle 9.
Belle anabainisha vigezo vya kufanya kazi na wasanii wa kimataifa kuwa ni pamoja na shoo kubwa alizowahi kufanya msanii awali.  “Vigezo vingine wanaangalia kazi na ‘performance’ yako ya home, wanaangalia unavyokubalika na mashabiki, ninachoamini mashabiki ndiyo majaji kwangu kuhusu vigezo hivyo,”anasema Belle 9.
Mkakati wa 2013
Belle anasema wakati akiendelea kusubiri ‘colabo’ na wasanii wa kimataifa, mwaka huu pia anatarajia kufanya kazi na wasanii mbalimbali, ambao tayari amefanya nao mawasiliano ya karibu.
“Kuna Wayre, Bebe cool na wengine wengi, ambao nitaandaa kazi kwa ajili ya kufanya nao. Lengo kubwa ni kuhakikisha napanua muziki wangu, kwani sanaa ya bongo haitaweza kutimiza malengo yangu,”anasema Belle 9.
Anasema kuwa hatua hizo ameanza kuzitekeleza, baada ya kufanya colabo na msanii nyimbo za raga’ maarufu kwa jina Kanball kutoka nchini Kenya
“Nimefanya naye kazi moja inaitwa ‘demu wangu’, ambayo itatoka hivi karibuni. Ninataka kuitengenezea video ndiyo niitoe, siwezi kusema itakuwa lini,”anasema Belle 9.
Anabainisha kuwa anatamani siku moja kuingia studio na kufanya kazi na wazalishaji wakongwe (Maproducer) wakiwamo, P Funk Majani, Duke, Timberland na Mona Gangstar.
Maisha yake
Belle 9 ni mzaliwa wa Iringa mjini miaka 24 iliyopita, ambaye maskani yake iko Morogoro. Mbali na kazi zake nyingi kuzifanyia jijini Dar es Salaam akiwa na bado  anaishi maisha ya ukapela.
Anasema kuwa mbali ya muziki, hakuna chochote anachojishughulisha nacho kwa sasa mbali na kazi ya muziki.

SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment