Baada ya taarifa za msiba kusambaa kila sehemu Africa na dunia kuhusu
kifo cha mwanamuziki Goldie Harvey, hatimaye aliyekuwa mume mtarajiwa wa
marehemu Goldie, Prezzo ameonyesha kuguswa kwake na kifo hicho cha
mpenzi wake.
Prezzo ameandika maneno katika ukurasa wake wa facebook yakionesha ni
jinsi gani ameguswa na msiba huo. Hapa chini ndio maneno aliyoandika
msanii huyo...

Huu Ndio Ugonjwa Uliopelekea Kifo Cha Mwanamuziki Goldie Harvey...

Marehemu Goldie Harvey ambaye alikutwa na mauti,kuwafanya mashabiki wake kushikwa na simanzi kubwa kuhusiana
na taarifa za kifo chake imeelezwa kuwa ugonjwa wa ''Pulmonary
Embolism'' ndio uliopelekea kifo chake.
Ugonjwa huo unaosababishwa na kuganda kwa damu, husababisha mshipa
mkubwa ambao unasafirisha damu na hewa kwenda kwenye mapafu kuziba na
kupelekea binadamu kufariki ghafla.
0 comments:
Post a Comment