VURUGU ZINAZOENDELEA KIBITI RUFIJI SASA HIVI, WANANCHI WAMEVAMIA POLISI, WANACHOMA KITUO CHA POLISI NA NYUMBA ZA POLISI



.
Mwandishi Mrokim wa Father Kidevu Blog anaripoti kwamba kundi la wananchi wenye hasira wamevamia kituo cha Polisi Kibiti Wilayani Rufiji na kuleta vurugu kubwa kutokana na raia mmoja kufa kwa kile kilichodaiwa kuwa kipigo cha Polisi.
Aliyefariki ni Hamis Mpondi ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu Muhimbili.
Habari za sasa ni kwamba wananchi hao wanateketeza nyumba za Askari Polisi  zilizopo jirani na kituo hicho licha ya juhudi za Polisi kuwatawanya kwa mabomu, pia wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe magogo na kuchoma matairi ikiwa ni umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti, hali inaelezwa kuwa inazidi kuwa tete huku Polisi wa Kibiti wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu hewani kujaribu kutawanya watu.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment