Msanii Ricky Ross, leo asubuhi amenusurika kifo baada ya mtu mmoja
aliekua na silaha kurusha risasi kadhaa kwenye gari aina ya Rolls Roys
aliyokuwemo Ross na dem mmoja Ft. Lauderdale, Florida na kusababisha
kugonga nyumba akijaribu kuongeza mwendo.
Ross hakupatwa na risasi hata moja wakati wa tukio hilo wala dem aliekuwa nae ndani ya gari hilo.
Ripoti zinadai risasi kibao zilirushwa kuelekea kwenye gari hilo mda wa
saa kumi na moja asubuhi, na hakuna hata moja iliyoshoot kwenye Rolls.
polisi wanasema gari lingine lilisimama karibu na gari la Ross na mtu
mmoja aliekuwa kwenye gari hilo kuanza kurusha risasi kwenye gari la
Ross
Mpaka sasa hakuna alietuhumiwa, kugundulika wala kushikiliwa juu ya tukio hilo
0 comments:
Post a Comment