Chilla akiongea katika kipindi cha Makutano Magic FM...

Muendeshaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango akiwa na QChilla na mwanae Nuru baada ya kipindi
Q
Chilla amesema kuingia kwake kwenye matumizi ya madawa ya kulevya
ilisababishwa na baadhi ya watu kuchangia kumrudisha chini na kujikuta
yuko peke yake katika mitihani aliyokuwa akipitia.
Huku
akikataa kuwataja kwa majina alisema watu hao walihakikisha kila
anachokifanya hakifanikiwi na kujikuta katika wakati mgumu.
Akiongea na Fina Mango kwenye kipindi cha Makutano, Qchilla amesema alishindwa kujua amemkosea nani au nani amuombe msamaha.
Hata
hivyo anasema anawashukuru watu wake karibu waliokuwa wakisikitishwa na
hali aliyokuwa nayo na kuamua kumshauri aache kutumia madawa hayo.
Alipoulizwa
anawashauri vipi wasanii ambao wametumbukia kwenye matumizi hayo
alisema njia pekee ni kukubali kuwa wana tatizo na kuishika dini.
Pia
aliipongeza hatua ya rais Kikwete kumsaidia Ray C ambaye pia alikuwa
aliingia katika wimbi hilo akitolea mfano wa rais Nelson Mandela
aliejaribu kumsaidia mwanamuziki Brenda Fassie na Rais Obama aliemsaidia
marehemu Whitney Houston na kusisitiza wasanii wote ambao ni waathirika
wa madawa ya kulevya kujitokeza ili wasaidiwe na jamii.
QChilla
amesema kwa sasa anafanya muziki akilenga soko la kimatafifa zaidi
akiwatolea mfano PSquare na kusema tatizo la wanamuziki wengi kuishia
kusikika nchini tu ni kujiwekea mipaka na kulenga soko la ndani tu na
kumalizia hana mpango wa kutoa album badala yake ataendelea kutoa nyimbo
kali.
0 comments:
Post a Comment