Mwishoni mwa mwaka jana kiwanda
cha muziki Afrika kilipata taarifa za P Square wa Nigeria kumtimua
kwenye lebo yao msanii May D ambae alikula shavu kwenye kolabo ya chop
my money, ikawa ishu ambayo ilizungumzwa sana kwenye media na beef
ikaonekana waziwazi.
Baadae May D alizungumza na
kusema taarifa za kufukuzwa kwake kwenye lebo ya P Square alizisikia tu
kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari lakini kina P Square
hawakuwahi kumueleza chochote kitu ambacho kilimpa mwamko wa
kuwashitaki.
Baada ya hapo kila mtu alijua
kuna beef zito lakini siku chache zilizopita imeanza kuonekana kwamba
hawako tena kwenye beef ambalo walikua hata hawaongei, juzi wakati May D
amepata mtoto wa kiume Peter wa P Square aliamua kumuandikia kupitia
twitter na kumpa hongera, hiyo ni moja ya ishara kwamba sasa hivi kuna
uhusiano ambao sio mbaya kati yao japo pia itakua poa tukisikia kutoka
kwao.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment