Msanii nyota wa filamu nchini na
aliyekuwa Miss Tanzania 2006/07 Wema Isack Sepetu katikati ya wiki
iliyopita alilitia aibu kundi la bongo muvi kwa kufanya kitu cha kipekee
kwenye msiba wa mwanamuziki na msanii wa komedi aliyefariki kwa ajali
Mkoani Tanga Sharo Milionea.
Wema Sepetu ambae siku za hivi
karibuni amepumnzika skendo kwenye vyombo vya habari alipongezwa na
watu kwa uungwana aliounonesha baada ya kutoa mchango mwingi kuliko
msanii yeyote wa kundi hilo linalosifika kwa kashfa za ngono.
Habari zilizothibitishwa na mmoja wa
ndugu wa marehemu ambae aligoma kutaja jina lake kwa madai kuwa yeye si
msemaji wa familia alisema kuwa” Ni kweli wasanii mbalimbali walijitolea
kwa kuja huku Tanga lakini Wema ndiye aliyetoa mchango mkubwa sana kwa
kutoa shilingi laki mbili peke yake 200000/= huku wasanii wengine
wakiishia kutia aibu”Alisema mtu.
Aidha ilidaiwa Wema ndiye aliyeonekana
kuwa na uchungu wa dhati toka moyoni ambapo licha ya mchango huo pia
alionekana kujishughulisha na kazi za kusaidia majukumu msibani hapo
bila kujali ustaa wake aliokuwa nao.
0 comments:
Post a Comment