Habari za siku nyingi
Ndugu, jamaa na marafiki.
Ni matumaini yangu wote mu wazima wa afya tukiwa tunaelekea kuumaliza 2012.
Nina jambo napenda kuwajulisha ambalo naona ni kheri tukishiriki sote pamoja kama watanzania.
Yeyote mwenye kuguswa na atakaeona ni vema kushiriki basi anakaribishwa.
Kila siku nikiamka nyumbani iwe ni asubuhi, mchana au jioni nimekuwa nikikuta barua si chini ya 5
Zote zikiwa ni za kuomba misaada mbali mbali. Kazi, Ada za shule, Chakula, muziki n.k
Mbali na Barua hizo, pia nimekuwa nikipokea mails mbali mbali pia za watu wanaohitaji msaada.
Nimeona kiukweli mimi siwezi kusaidia peke yangu kutokana na wingi wa barua hizo, kulinganisha na uwezo halisi nilio nao.
Wazo lililonijia ni kuweka barua na e mail hizo hapa
Zisomwe na watu mbali mbali
Ili kama kuna itakaemgusa, atakae ona anaweza kusaidia moja wapo ya barua hizo basi na afanye hivyo ili kushika mikono walio chini ki uwezo.
Nitajitahidi ku post walau barua 2 -3 au email 2-3 kwa wiki
Nikipata muda, manake Diary inabana mpaka blog nishaisahau
Inawezekana wapo wasanii, yani wanaoomba lakini si kweli kuwa wana matatizo hayo
Na pia inawezekana kabisa kuwa wapo wenye shida na wanahitaji kusaidiwa.
Itakuwa ni jukumu la anaetaka kutoa msaada kufatilia na kujua ukweli halisi kutoka kwa muombaji, kwakuwa maombi mengi huambatana na namba za simu za muombaji au e-mail yake.
0 comments:
Post a Comment