baby madaha nusu kufa

Msanii wa filamu ambaye pia anafanya muziki Baby Madaha, amendoka ghafla wakati akishuti filamu yake mpya na kupoteza fahamu ambapo sasa amelazwa kwenye hosptali Amana jijini Dar es Salaam, na habari zinadai kuwa msanii huyo anasumbuliwa na ugonjwa wa kuanguka.

Chanzo cha habari ambacho kipo katika hosptali hiyo kilidai kuwa msanii huyo kwa sasa huwezi kuzungumza kwani bado hali yake si nzuri na amepewa muda wa kupumzika bila kufanya kazi yoyote akiwa chini ya usimamizi.

Hata hivyo kwa mujibu wa daktari ambaye anamtibu Madaha alitoa taarifa kuwa msanii huyo wakati anapiga picha za filamu hiyo alikuwa hajala chakula chochote badala yake alitumia kinywaji kikali kitu ambacho kiliamsha tatizo lake lake.

Kwa mujibu wa madaktari wanadai kuwa ni kweli Madaha anasumbuliwa na ugonjwa wa kuanguka lakini pia tatizo liilichangiwa na unywaji wa pombe kali kabla hajala hivyo kwa sasa bado anafanyiwa vipomo ili kuona kama kuna tatizo lingine.
SHARE

Milan Tomic

Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment