Mhe.Lily Munanka (kulia) akisalimiana na Balozi Roubani Kaambi wa Visiwa vya Comoro Ubalozini Tanzania House Washington DC.
Mhe.Balozi Roubani Kaambi wa Visiwa vya Comoro katika picha ya pamoja na Mhe.Lily Munanka, Kaimu Balozi.
Mhe.Balozi Roubani Kaambi wa Visiwa vya Comoro akisalimiana na Suleiman Saleh,(kulia) Afisa Ubalozi wa Tanzania,Washington DC.
Mhe.Balozi Roubani Kaambi wa Visiwa vya Comoro (katikati) katika
picha ya pamoja na Suleiman Saleh,(kulia) Afisa Ubalozi wa
Tanzania,Washington DC. Kushoto ni Mhe.Lily Munanka Kaimu Balozi.
Balozi wa visiwa vya Comoro nchini Marekani Mhe. Roubani Kaambi jana
alitembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania (Tanzania House)
Washington DC na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi Mhe. Lily Munanka
ambayo yalilenga katika kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili.
Balozi Roubani ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Visiwa vya Comoro
katika Umoja wa Mataifa alisisitiza umuhimu wa Tanzania na Comoro
kuimarisha zaidi mahusiano yao kihistoria na kuyatafsiri mahusiano hayo
katika mashirikiano zaidi kiuchumi. Balozi Roubani alibainisha kwamba
nchi yake inafahamu mafanikio mbali mbali katika sekta za uwekezaji
pamoja na utalii na hivyo kuomba nchi yake isaidiwe kuwavutia
wawekezaji kutoka Marekani pamoja na kukuza utalii kutokana na mazingira
ya nchi yake kufanana na yale ya Tanzania Bara na Visiwani.
Kwa upande wake Kaimu Balozi Mhe. Lily Munanka alimshukuru Balozi Kaambi
kwa kumtembelea na kumweleza kwamba kimsingi ameyapokea maombi yake
hayo na atayawasilisha katika mamlaka husika ili yatolewe maamuzi
stahili. Kwa ujumla Kaimu Balozi Munanka alimhakikishia Balozi Kaambi
kwamba Tanzania inathamini mahusiano baina ya nchi zao na kuona umuhimu
wa kujenga mashirikiano zaidi kiuchumi baina ya nchi zao mbili kwa faida
ya wananchi wao,
Hi. I’m Designer of Blog Magic. I’m CEO/Founder of ThemeXpose. I’m Creative Art Director, Web Designer, UI/UX Designer, Interaction Designer, Industrial Designer, Web Developer, Business Enthusiast, StartUp Enthusiast, Speaker, Writer and Photographer. Inspired to make things looks better.
0 comments:
Post a Comment