KAJALA APIGA TATUU YENYE JINA LA WEMA MGONGONI MWAKE
Baada ya hivi karibuni msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu kumlipia
Kajala Masanja faini ya shilingi milioni 13 ili asiende jela kwa kesi
iliyokuwa ikimkabili, Kajala ameamua kulipa fadhila kwa kujichora tatuu
ya jina la Wema mgongoni mwake.
Akizungumza na Ijumaa juzi kuhusiana na uamuzi huo, Kajala alisema
Wema amemfanyia kitu kikubwa sana kiasi kwamba amefikiria cha kumlipa
bila majibu hivyo akaamua kujichora tatuu hiyo ambayo itamfanya
amkumbuke daima.
“Kwa kweli Wema amenifanya kitu kikubwa sana, nyie wenyewe ni
mashahidi. Nimefikiria nimlipe nini kwa fadhila zake hizo, nikakosa jibu
na ndipo nikaamua kujichora tatuu hii ambayo haitafutika mwilini mwangu
maisha,” alisema Kajala.
0 comments:
Post a Comment