Dar es Salaam. Wafanyakazi wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wameulalamikia uongozi wa hospitali hiyo
kwa kushindwa kupeleka michango yao wanayokatwa kwenye mishahara kwa
ajili ya kulipia Mfuko wa wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Wakizungumza kupitia baruapepe waliyouandikai
uongozi huo (nakala tunayo), wafanyakazi hao wamedai kuwa michango hiyo
haijapelekwa tangu Oktoba mwaka jana hadi Januari 2013 hivyo kuwakosesha
haki ya matibabu.
“NHIF haijapata michango ya asilimia tatu tangu
Oktoba mwaka 2012 hadi Januari 2013, kwa mantiki hiyo basi huduma
nyingine kama kupokea fomu na kubadilisha kadi hazitolewi pamoja na
vibali na vipimo ni ndoto kwa sasa,” imesema sehemu ya barua hiyo.
Hata hivyo barua hiyo imeongeza kuwa, Serikali
imeshalipa sehemu yake kumchangia mfanyakazi lakini kwa upande wa
hospitali hiyo ndiyo bado haijalipa.
Wafanyakazi kupitia barua hiyo wamemtaka
Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo kumwagiza mkaguzi wa ndani kufanya
ukaguzi wa akaunti inayohusu malipo hayo ili ili kubaini ukweli wa
jambo hilo.
Alipotafutwa kwa njia ya simu, Mkurugenzi Mtendaji
wa hospitali hiyo Dk Marina Njelekela alikataa kuzungumzia suala hilo
na kumtaka mwandishi amtafute ofisa habari. Naye Ofisa habari wa
hospitali hiyo Eligaesha Buberwa alikiri kuwepo kwa tatizo hilo lakini
akapinga kuwa limeanza tangu mwaka jana.
“Siyo kweli kwamba tatizo hilo lilianza Oktoba
mwaka 2012. Ni kweli tuna deni la Machi mwaka huu. Unajua wale NHIF wana
utaratibu wa kukatisha huduma kama usipolipa tarehe 5 ya mwezi mmoja
mbele,” alisema Eligaesha
0 comments:
Post a Comment